Breaking News

HABARI PICHA UZINDUZI WA SHIRIKA LA WOMEN DREAM FULFILMENT ULIOFANYIKA MKOANI MWANZA.

Na Tonny Alphonce,Mwanza.

Shirika la Women Dream Fulfilment limezinduliwa rasimi Mkoani Mwanza, shirika hili lilianzishwa mwaka 2019 likiwa kama kikundi cha vijana wa kike watatu waliokuwa wakijishughulisha na kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao katika masomo.

Kwa sasa shirika la Women Dream Fulfilment limejikita katika kuwawezesha wanawake kiuchumi ili kutimiza ndoto zao kupitia sekta ya Uvuvi,Ujasiriamali,Kilimo,Madini,Utalii na Teknolojia ya Habari.


Mkurugenzi wa Shirika la 
Women Dream Fulfilment Madame Vcky John akitoa utambulisho wa wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya kufanyika kwa uzinduzi.


Mgeni Rasimi katika uzinduzi wa Shirika la Women Dream Fulfilment akifurahia jambo kabla ya kulizindua rasimi shirika hilo.


Wakili Msomi Jacqueline akitoa Mada juu ya Fursa zilizopo kwa wale watakaoamua kujiunga na klub ya Women Dream.


Baadhi ya washiriki wakifatilia matukio mbalimbali katika uzinduzi wa 
Shirika la Women Dream Fulfilment .

Dr. B.S. Nyabweta – Katibu Mtendaji wa Shirika la Women Dream Fulfilment akitoa neno la utambulisho wa WDFF.


Mgeni rasimi akisikiliza mpango na ndoto za shirika 
 la Women Dream Fulfilment mara baada ya kuzinduliwa.

Shirika kwa sasa limeanza utekelezaji wa program ya mafunzo ya utunzaji wa takwimu za afya kwa mfumo wa teknolojia kama sehemu ya kuwaandaa watakwimu wasaidizi wanawake (Assistant Data Clerk) ambao kimsingi wanahitajika sana kwenye eneo la afya hapa nchini.

Program hiiambayo ni muhimu sana na ndiyo kipaumbele kikubwa kwa shirika hili na Kwa sasa zaidi ya  vijana arobaini (40) wataenda  kunufaika na program hiyo


No comments