Breaking News

Vijana wahimizwa kusomea mionzi

Rais wa Chama cha wataalamu wa mionzi Tanzania Baraka Msongamwanja akizungumza na waandishi wahabari

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Wataalamu wa mionzi wakutana Jijini Mwanza kwa lengo la kuendelea  kubadirishana ujuzi na kukumbushana wajibu wa kazi zao.

Hayo ameyasema raisi wa chama cha wataalamu wa mionzi Tanzania(TARA) Baraka Msongamwanja alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano  wa maadhimisho ya kongamano la wataalamu wa mionzi Tanzania uliofanyika Mkoani hapa uliowakutanisha wananchama zaidi ya 3000 wenye lengo la kukumbushana majukumu na namna ya kuiboresha taaluma hiyo.

Msongamwanja amesema kuwa taaluma yao inahusika na uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kama Kansa ili kuweza kubaini tatizo la mgonjwa husika na kupatiwa matibabu kutokana na majibu ya vipimo.

Ameongeza kuwa kwa sasa Watanzani wengi wameelewa umuhimu wa kufanya vipimo vya mionzi tofauti na zamani ambapo wananchi wengi walikuwa hawajatambua thamani ya vipimo hivyo ambavyo vinasaidia kugundilika kwa maradhi.

"Hapo swali muitikio ulikuwa siyo hivi unakuta mtu anafika hospitali ukimwambia akadange ultrasound anasura anasema unataka nipunguze maisha yangu lakini kwasasa mwanamke akibeba mimba tuu ndani ya wiki moja anataka kuja kupima ili apate uhakika na hata hivyo Serikali imeboresha sana katika vifaa bora kwa sasa hivi unavyozungumzia Tanzania kipimo cha RMI kinapatikana hapa Nchini kwetu amesema Bakari.

Nae Faustine Mulyutu Mratibu wa huduma za mionzi Mkoa wa Shinyanga  amesema kuwa,mwaka 2021 Serikali imeweza kutoa mashine za Kupimia mionzi kwa mikoa yote Tanzania hivyo ni vema kupatikana wataalamu wamionzi  ili waweze kutoa huduma kwa wagonjwa.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Ultrasound  Saada  Kasuwi ametoa rai kwa jamii kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara ili kuweza kubaini shida walizonazo na kuweza kupata tiba mapema na ameiomba serikali kutoa nafasi za ajira ilikupunguza uhaba wa wataalamu.

amesema kuwa vijana hususani wa kike wajitokeze kwa wingi  kusome fani ya mionzi ili waweze kuongeza idadi ya wataalamu watakao isadia Jamii na Taifa kwa ujumla.

Amesema vijana wengi wanahitaji kupatiwa elimu juu ya kutambua umuhimu wa kusomea masomo ya mionzi kwani wengi wao wanaona kuwa ni masomo magumu sana na hivyo kufanya idadi ya wanafunzi kuwa ndogo katika vyuo vinavyohusika na masomo hayo.

Mwishoo

No comments