Breaking News

MWANAMUZIKI FERRE GOLA KUTOA BURUDANI SIKU YA X MASS MWANZA.

 Mwandishi Wetu,Mwanza

Mwanamuziki Ferre Gola kutoka Congo anatarajiwa kuwasha moto Siku ya X Mass Mkoani Mwanza.


Hii ni mara ya kwanza kwa mwanamuziki Ferre Gola kutumbuiza Mkoani Mwanza ambapo amesema atatoa burudani itakayoacha historia kwa mashabiki wa muziki wa dance nchini.


Mratibu wa onyesho hilo kutoka Rena Events Jacob Usungu amesema wakazi wa Mwanza wategemee burudani nzuri na yatofauti.

'Huyu ni mwanamuziki mkubwa sana kule Congo na Afrika kwa ujumla kwa maana hiyo ni bahati kubwa kwa wakazi wa Mwanza kumshuhudia mwamba huyu akiwa katika jukwaa hapa Mwanza.alisema Usungu'

Usungu amesema akiwa hapa nchini Ferre Gola atatumbuiza jijini Dar es Salaam tarehe 24/12/2021 na kumaliza Jijini Mwanza tarehe 25/12/2021 katika Hotel ya Malaika.

Tiketi kwaajili ya onyesho hilo zitaanza kuuzwa tarehe 22/12/2021 katika maeneo Weekend Car Wash Nyegezi,Yuhoma Educational Ltd Jengo la Nyanza,Sato Sangala Lakairo Kirumba,Frolah Sloon na Malaika Hotel.

No comments