Breaking News

Spika mstaafu azindua mfumo wa anwani ya makazi Jijini Mwanza

Na Hellen Mtereko, Mwanza

Matumizi ya mfumo wa anwani ya makazi umezinduliwa rasmi Kitaifa  leo Desemba 3,2021katika Mkoa wa Mwanza.


Sipika mstaafu Anna Makinda akizindua matumizi ya mfumo wa anwani ya makazi leo Desemba 3,2021 katika viwanja vya Shule ya msingi Buhongwa 'B' iliyoko Jijini Mwanza

Uzinduzi huo umefanywa na spika mstaafu Anna Makinda wakati akizungumza na Wananchi juu ya matumizi ya anwani ya makazi katika viwanja vya Shule ya msingi Buhongwa 'B'.

Amesema kuwa mfumo huo utawasaidia Wananchi kutambulika kwa urahisi katika maeneo yao sanjari na kurahisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii. 

Amesema kuwa anwani ya makazi ni muhimu Sana katika Jamii kwani inarahisisha shughuli za kibiashara kuwafikia majumbani kwa urahisi na hivyo kupelekea uchumi wa mtu mmoja mmoja kukua kwa haraka.


Sipika mstaafu Anna Makinda akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel anwani ya makazi mara baada ya uzinduzi.


Wananchi waliohudhuria kwenye hafla ya uzinduzi wa matumizi ya mfumo wa anwani za makazi

No comments