Breaking News

EMEDO NA RNLI WAJA NA MRADI WA KUPUNGUZA AJALI ZA KUZAMA MAJINI KWA JAMII YA WAVUVI.

 Na Tonny Alphonce,Mwanza.

Imeelezwa kuwa Jamii za Wavuvi laki moja wanaofanya shughuli zao na kuishi pembezoni mwa  Ziwa Victoria ,Mia mbili Thelathini na Moja kati yao wanapoteza Maisha kwa mwaka kwa kuzama majini.

Mkurugenzi  Mtendaji wa EMEDO Editrudith Lukanga na Steve Wills Mkuu wa program RNLI wakitia Saini ya Mkataba wa miaka mitatu wa kutekeleza mradi wa kupunguza ajali za kuzama majini katika Ziwa Victoria

Idadi hiyo ya vifo huenda ikapungua kutokana na Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo Tanzania EMEDO na Taasisi kutoka Wingereza inayohusika na masuala ya usalama kwenye maji na uokoaji RNLI kuingia mkataba wa miaka mitatu wa kusaidia jamii za wavuvi.

Mratibu wa Mradi huo Arthur Mugema amesema EMEDO NA RNLI wamekubaliana kupitia mradi huo wa miaka mitatu waweze kufikia  matokeo ya jumla hadi ifikapo 2025 na kuona wadau wakichukua hatua zinazofaa katika kupunguza matukio ya watu kuzama majini hasa kwa jamii inayoishi pembezoni mwa Ziwa Victoria.


Mratibu wa Mradi Arthur Mugema akielezea namna mradi huo utakavyofanyakazi na kuwa msaada mkubwa kwa Jamii ya Wavuvi.

Arthur amesema Mradi huu utatekelezwa katika vijiji 7 ambavyo vilichaguliwa kutokana na utafiti uliofanywa na kuvitaja vijiji hivyo kuwa ni visiwa vya Gozba na Mulumo vinavyopatikana Wilayani Muleba,Musozi na Irondo vinavyopatikana Ukerewe,Kome na Busekela katika Hlmashauri ya Wilaya ya Musoma na Sweya iliyopo Nyamagana Jijini Mwanza.

kwa upande wake Mkurugenzi  Mtendaji wa EMEDO Editrudith Lukanga amesema mradi huu ni kwanza  kufanyika Afrika ukiwa umelenga kutoa usalama kwa jamii za wavuvi wanaofanya kazi majini na waleo wanaoishi pembezoni mwa Ziwa Victoria.


Mkurugenzi  Mtendaji wa EMEDO Editrudith Lukanga akizungumzia namna mchakato ulivyoanza hadi kufikia tukio la kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanya mradi huo wa kipekee Afrika.

Bi Lukanga amesema mradi huu pia unatekeleza sera mbalimbali zilizopo ambazo zinasisitiza suala la usalama wa wavuvi pamoja na suala la uvuvi endelevu.

 Amesema mradi huu sasa hautaangalia Samaki tu kama rasilimali lakini sasa mradi huu utawaangalia watu ambao ni  wavuvi kwa sababu bila watu hata uvuvi wenyewe unaweza usiwepo.

 Niseme tu tunabahati kubwa sana kwa sababu tumesaini mradi huu kipindi hizuri  kwa sababu mwaka 2022 umetambulika kama mwaka wa kimataifa kuwa mwaka wa kimataifa wa wavuvi mdogo na ufugaji wa viumbe majini na una misingi yake na mradi huu unaingia huko.alisema Bi Lukanga

Naye Steve Wills Mkuu wa program RNLI amesema mradi huu ni muhimu sana kwa sababu tafiti mbalimbali zinaonyesha watu wengi wanaofanya kazi za majini na wanaoishi pembezoni mwa maji wanapoteza maisha na kuziacha familia zikiwa hazijui nini cha kufanya.


Steve Wills Mkuu wa program RNLI akizungumzia sababu zilizopelekea RNLI kutoa fedha za kutekeleza mradi huu wa kupunguza ajali za kuzama majini kwa Jamii ya Wavuvi

Amesema kupitia mradi huu anaamini maisha ya jamii ya wavuvi itapatiwa elimu na hivyo itaweza kujilinda na kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vinavyotokana na kuzama majini. Picha zote na Dr Tonny.

No comments