Takukuru Yawanoa Skauti kupingana na rushwa Tanzania.
Na Maridhia Ngemela, Mwanza.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) kwa kushirikiana na chama cha skauti Mkoani Mwanza wametoa mafunzo kwa walimu walezi,viongozi wa makundi ya skauti kwa lengo la kuwapatia elimu juu ya mapambano zidi ya rushwa.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala akifungua mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yamefanyika Machi 30,2022 Jijini Mwanza katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Jiji la Mwanza.Kaimu Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Nyamagana, Innocent Shetui alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa semina hiyo amesema kuwa kupitia mkakati wa Takukuru na skauti( TAKUSKA) wenye kauli mbiu isemayo "Tokomeza rushwa" wametoa elimu hiyo kwa walimu walezi ili wakawafundishe vijana namna bora na mbinu muhimu za kushiriki kwenye mapambano zidi ya rushwa.
Amesema vijana walioko mashuleni wakiandaliwa vizuri Jamii ya Kitanzania itakuwa salama kutokana na kutengeneza kizazi kitakachokuja kutumikia Taifa lisilokubali rushwa na kukataa kutoka moyoni kutokana na malezi na elimu waliyoipata kutoka kwa walimu.
Nae Kamishina wa skauti Mkoa wa Mwanza Wande Munkyala amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa salama juu ya kutokomeza rushwa hivyo kila shule kuanzia ngazi ya awali hadi msingi watengeneze vilabu vya kutoa elimu kwa watoto hao.
Amesema mafunzo hayo ni mpango wa Taifa hivyo amewataka walimu wanaopatiwa mafunzo hayo kuendeleza mpango wa skauti mashuleni ili kuwafichua wanao toa na kupokea rushwa kwani vijana wakianza kufundishwa bado wadogo inakuwa ni chachu ya kuleta mabadiliko na kupandikiza roho ya kuchukia vitendo hivyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala aliyekuwa mgeni rasmi katika semina hiyo aliyemuwakilisha mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi amesema kuwa mafunzo hayo yamekuja muda sahihi kabisa ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu ameelekeza fedha nyingi katika miradi ya ujenzi, hivyo kupitia elimu mtakayoipata ninaimani mtakuwa mabolozi wazuri wa kuielimisha jamii juu ya kuachana na vitendo vya rushwa.
Amesema malezi bora yanaendana na mkakati huu wa kupambana na rushwa ni vema kuendelea kutengeneza timu ya pamoja itakayo saidia kupitia mafunzo haya mkawafunze vijana madhara na faida za kupinga rushwa ili tuwe na Taifa lenye kupambania maendeleo kwani rushwa ni adui wa maendeleo na inakaribisha umasikini.
No comments