Breaking News

OJADACT WAWAPIGA MSASA WANAHABARI KATIKA KURIPOTI HABARI ZA MAZINGIRA

                            Na Tonny Alphonce,Mwanza

Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT)  na Shirika la Kimataifa la  Environmental Reporting Collective la Nchini Malaysia (ERC) limeendesha mafunzo ya siku moja ya  Uandishi wa Habari za Uchunguzi upande wa Sekta ya Uhifadhi wa Mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.


Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred akifungua mafunzo ya siku moja Uandishi wa Habari za Uchunguzi upande wa Sekta ya Uhifadhi wa Mazingira kwa waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza.
(picha na Dr Tonny)

Akizungumza wakati alipokuwa akifungua mafunzo hayo Mgeni rasmi  Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Mhe. Yonas Alfred kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Hassan Masala amewataka waandishi wa habari kuwa wabobezi katika uandishi wa habari za aina moja ili habari hizo ziwe na tija kwa jamii.

'Mkoa wetu wa Mwanza bado unachangamoto za kimazingira,kuna uvuvi haramu,kunaukataji hovyo wa miti hizo zote ni habari ambazo mnatakiwa kuziandika na zitakuwa na msaada mkubwa kwa jamii'.alimesema Alfred.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko amesema amewataka wanahabari hao kutumia mafunzo waliyoyapata kuibua uharifu wa mazingira ambao unaendelea.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko akiongea na wanahabari hawapo pichani.
(picha na Dr Tonny)

'Najua kunachangamoto za kisheria bado tunazo hivyo ni vizuri tuzisome sheria hizi na kuzielewa lakini kama utaona sheria inakubana angalia namna ya kuripoti habari hiyo.'alisema Soko. 

Baadhi ya Wanahabari wakifatilia moja ya mada iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko.
(Picha Malunde Blog)
Jumla ya wanahabari 20 wamepatiwa mafunzo ya namna ya kuripoti habari za uhalifu wa kimazingira ili waweze kuwa chachu ya kufatilia na kuripoti habari za Mazingira,pia mafunzo hayo yafatiwa na mafunzo mengine yatakayo washirikisha waandishi habari 20 kwa njia ya mtandaoni april 9 mwaka huu.No comments