Breaking News

Tuweke mifumo mizuri katika sekta ya habari.



Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Serikali ya Marekani imehaidi kuendelea kutoa msaada na ushirikiano kwa vyombo vya habari hayo yamebainishwa katika kongamano la Kuelekea siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Nchini na miaka sitini ya uhusiano wa kidplomasia Kati ya Tanzania na Marekani lililofanyika Mkoani Mwanza katika kampusi ya chuo kikuu cha Malimbe.



Mkuu wa kitengo cha habari kutoka Ubalozi wa Marekani Michael Pryor aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo amesema kuwa,Serikali ya Marekani imehaidi kuendelea kutoa msaada na ushirikiano kwa vyombo vya habari Tanzania.

Pryor ameongeza kuwa lengo la kuendelea kutoa msaada ni kuwawezesha waandishi wa habari ili waweze kuandika habari zenye tija.

Kwa upande wake Mtafiti kutoka Taasisi ya tafiti za uchumi na kijamii (REPOA) Steven Mwombela amesema kuwa Kuelekea siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambayo hufanyika kila mwaka ya Mei 3 ni vema waandishi wajikite zaidi kuandika habari za tija,uchunguzi na matumizi ya takwimu ili kuibua na kuendelea kuielimisha jamii.


Naye Godwin Asenga aliyekuwa mkufunzi katika mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika siku mbili Mkoani hapa amesema kuwa,lengo la kuhadhimishwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari Nchini ni kuikumbusha Serikali na wadau kuweka mifumo mizuri katika sekta hiyo.

Asenga amesema kuwa,takwimu za mwaka 2021 mach zinaonesha watumiaji wa intaneti wameongezeka kufikia million 70 kwa mujibu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania

No comments