Breaking News

MAKAPUNI 40 YAKIGENI KUSHIRIKI MAONYESHO BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI MWANZA

 

Na Tonny Alphonce,Mwanza.

 Jumla ya wafanyabiashara 390 wa ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki maonyesho ya biashara ya Afrika Mashariki kwa mwaka huu 2022 mkoani Mwanza.

Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoa wa Mwanza Gabriel Mugini Chacha akizungumza na Waandishi wa habari hawapo pichani.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara,Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoa wa Mwanza Gabriel Mugini Chacha  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chemba hiyo ambapo  wafanyabiashara 350 ni kutoka hapa nchini na wafanyabiashara 40 ni kutoka nje ya Tanzania.

Baadhi ya viongozi wa TCCI mkoa wa Mwanza wakiwa katika picha ya pamoja.

Bw Chacha amesema katika maonyesho hayo yatakayofanyika katika uwanja wa Nyamagana Mkoani Mwanza kuanzia tarehe 26/08/2022 hadi 04/09/2022 wafanyabishara kutoka nchi za afrika mashariki za Kenya,Uganda na Burundi na nchi za China,India na Indonesia watashiriki maonyesho hayo

 'Tunatarajia zaidi ya wananchi 250,000 watatembelea maonyesho haya kwa mwaka huu na kwa kweli watanufaka na huduma mbalimbali za taasisi za serikali zitakazokuwa zinapatikana lakini pia wananchi wataweza kujionea teknolojia mpya za mashine zinazohusiana bidhaa mbalimbali'.alisema Chacha.

 Akizungumzia fursa watakazozipata wafanyabiashara watakaoshiriki maonyesho hayo,Chacha amesema wafanyabiashara watanufaika kwa kuongeza mtandao wa kibiashara,kuongeza ubora wa bidhaa na kuongeza teknolojia,kupata masoko zaidi,makampuni ya kigeni kupata masoko na kubadilishana uzoefu.

 Nae katibu Mtendaji wa TCCIA mkoa wa Mwanza Hassan Karambi amesema maonyesho hayo yanafunguliwa rasimi tarehe 30/08/2022 na mkuu wa mkoa wa Mwanza  Mhe.Adam Malima.

Katibu Mtendaji wa TCCIA mkoa wa Mwanza Hassan Karambi akitoa akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari.

Karambi amesema sababu za maonyesho hayo kufanyikia katika uwanja wa Nyamagana kwa mwaka huu ni kuwapa fursa wananchi wa maeneo yote kushiriki bila tatizo lolote maonesho hayo kwa sababu uwanja huo upo katika ya jiji la Mwanza.


Huu ni mwaka 16 sasa TCCIA mkoa wa Mwanza wamekuwa wakiandaa maonyesho haya ya Biashara ya Afrika Mshariki na mwaka huu maonyesho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo lugha ya Kiswahili ni Nguzo ya Kukuza na kuendeleza Biashara,Viwanda na Kilimo Afrika.

 

No comments