Breaking News

UZINDUZI WA UTEKELEZAJI WA PJT-MMMAM MWANZA NI SEPTEMBA 22 MWAKA HUU

                                                      Na Tonny Alphonce,Mwanza

Wadau wa taasisi na mashirika yanayotoa huduma za watoto mkoa wa Mwanza wamekutana na timu ya waratibu wa PJT-MMMAM mkoa wa Mwanza kwa lengo la kujadiliana kuhusiana na matayarisho ya uzinduzi wa program hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 22/09/2023 mkoani Mwanza.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mratibu wa miradi elimu bwana Peter Matyoko kutoka Shirika la Uchumi wa Nyumbani (TAHEA) amewataka wadau hao kushiriki katika uzinduzi huo kwa kuwa ni muhimu kwa ustawi wa watoto wa Tanzania.


Mratibu wa Miradi elimu bwana Peter Matyoko kutoka Shirika la Uchumi wa Nyumbani (TAHEA) akisisitiza jambo wakati wa kikao Wadau wa taasisi na mashirika yanayotoa huduma za watoto mkoa wa Mwanza 

'Katika uzinduzi wa program hii tunatarajia mgeni rasimi atakuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza na wakuu wa wilaya wa halmashauri zote,Maafisa lishe,Wakurugenzi wote,Maafisa Elimu na Watu wa jenda nao watakuwepo kwa hiyo tunaomba tushikamane kufanikisha tukio hili'.alisema Peter

Peter amewataka wadau hao wanaotekeleza afua za ECD kuwatayari kwa kupokea ugeni utakaotoka katika halmashauri mbalimbali za mkoa wa Mwanza.

Baadhi ya wadau wa taasisi na mashirika yanayotoa huduma za watoto mkoa wa Mwanza wakifatilia kikao kilichowakutanisha na waratibu wa PJT-MMMAM.

Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Mwanza Janeth Shishila amewataka wadau hao pia kujiandaa kwaajili ya kupata mafunzo ya ECD ambayo yatawasaidia katika majukumu yao ya kuwahudumia watoto.

'Mafunzo haya ni mazuri sana mtaona wataalamu watakapokuja kuwafundisha sayansi ya ECD ya watoto kwa hiyo tujiandae tutapeana utaratibu wa namna gani tutafanikisha mafunzo haya mara baada ya uzinduzi wa PJT-MMMAM katika mkoa wetu wa Mwanza'.alisema Janeth 

Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Mwanza Janeth Shishila akizungumza na wadau wa taasisi na mashirika yanayotoa huduma za watoto mkoa wa Mwanza wakifatilia kikao kilichowakutanisha na waratibu wa PJT-MMMAM 

Janeth amezitaka taasisi hizo kuhakikisha kila shirika liwe na lengo la kumsaidia mtoto mwenye umri wa mwaka 0-8 ili kuifanikisha program hii ya taifa ambayo tayari imeanza kutekelezwa katika baadhi ya mikoa ya Tanzania.

Program ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto imeanza kutekelezwa katika baadhi ya mikoa hapa nchini,program hii ni ya kipindi cha miaka mitano 2021/2022 hadi 2025/2026

No comments