Breaking News

POLISI WATIBUA NDOA YA UTOTONI, MAHARI NG'OMBE WATATU

 

JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limevunja sherehe ya harusi ya msichana mwenye umri wa miaka 11.

Mtoto huyo alitarajiwa kuolewa jana kwa mahari ya ng'ombe watatu wilayani Same mkoani humo.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Simon Maigwa alisema tayari mtoto huyo alifanyiwa sherehe ya kumuaga (send off) Julai 7 mwaka huu nyumbani kwa wazazi wake kwenye Kijiji Cha Emuguri Kata ya Njoro wilayani Same.

Kamanda Maigwa alisema polisi wamemtia mbaroni baba mzazi wa mtoto huyo na kwamba jina la mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 68 na jina la aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa yamehifadhiwa kwa sababu za kiusalama.

"Polisi ilipata taarifa kutoka kwa raia wema juu ya kuwepo kwa harusi hiyo haramu nasi tukaandaa mtego ambao ulifanikisha kuvunja harusi hiyo" alisema.

No comments