Breaking News

UMASIKINI CHANZO CHA HUDUMA ZA AFYA YA AKILI KUTOPEWA KIPAUMBELE.

Na Blandina Aristides, Mwanza
.
 Imeelezwa kuwa Huduma za Afya ya akili hazijapewa kipaumbele kinachotakiwa kote Ulimwenguni na Katika nchi za uchumi wa Kati na Wa Chini ikiwemo Tanzania.
Mkuu wa Idara ya Afya  ya akili Dkt. Kiyetia Hauli akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani  uliofanyika Oktoba 07 Katika Hospital ya Rufaa ya Bugando Jijini hapa.

Hali hiyo imepelekea kutokuwepo kwa usawa kwenye maeneo ya upatikanaji wa huduma hiyo ambapo hupatikana kwenye miji Mikubwa pekee  na kwenye hospital Kubwa na si kwenye huduma za Msingi na jamii kama inavyotakiwa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Afya  ya akili Dkt. Kiyetia Hauli amesema Huduma hizo Mahali zilipo, mara nyingi zinalenga kwenye kutibu na si kukinga ubora wa huduma yenyewe.

Ameeleza kwamba huduma ambazo zimekua zikitolewa ni pamoja na  upatikanaji wa dawa, upatikanaji wa huduma za kisaikolojia na kijamii.

Anasema pia hazilengi kujua uhaba wa rasilimali watu wenye utaalamu wa Afya ya akili, upungufu wa sera,mipango, sheria na haki kwa watu wenye matatizo hayo Jambo ambalo huonesha  unyanyapaa, kutengwa na kudharauliwa na hatimae kupangwa kwa bajeti ndogo kwenye huduma ya Afya ya Akili.
Baadhi wananchi wakipata elimu juu ugonjwa wa Afya ya Akili katika viwanja vya Bugando Mkoani Mwanza.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa  maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani  uliofanyika Oktoba 07 Katika Hospital ya Rufaa ya Bugando Jijini hapa Dkt.Hauli ameeleza kuwa Ili kukabiliana na ukosefu huo wa usawa,  Shirika la Afya Duniani na Shirika la Afya ya akili duniani wanasisitiza na kulenga nchi husika na watalam wa Afya kuzingatia mikakati ambayo inalenga kuboresha na kukinga Afya ya akili kuanzia ngazi ya Chini.

  "Hii itafanikiwa Zaidi kwa kutoa ujuzi shirikishi kwenye huduma nyingine za Msingi kama vile huduma ya Mama na mtoto, CTC, Magonjwa sugu yasiyoambukiza na huduma za Afya kwa ujumla " alisema Hauli

Uzinduzi huo unaenda sambamba na kuelekea maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa hospital ya Rufaa ya Kanda Bugando ambapo utaambatana na kutoa huduma za kitabibu na ushauri bure kwa Muda wa siku tatu.

Kwa upande wake Daktari bingwa na mbobezi wa Wtoto na Vijana Gema Simbele ameeleza kuwa matatizo ya Afya ya Akili huanza wakati wa ujauzito ambapo huchangiwa na Umaskini na lishe duni anayopata mama wakati wa ujauzito.

Anasema asilimia 80 ya Ugonjwa huo niwa kurithi na asilimia 50 ya watu wazima wenye tatizo la Afya ya akili hutokea Kabla ya umri wa miaka 14 huku akiwataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wenye tatizo Hilo  kwenye vituo vya kutolea huduma iliwapatiwe matibabu na na kuhakikisha Afya zao zinaimarika. 

Mwisho.

No comments