Breaking News

HABARI PICHA,MKUU WA MKOA WA MWANZA ATEMBELEA KITUO CHA ICILD NA KUWATAKA VIJANA KUJIFUNZA LUGHA ZA KIGENI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Mhandisi Roberth Gabriel leo tarehe 22/11/2021 amekitembelea Kituo Cha Kimataifa Cha Lugha ,Utamaduni na Mendeleo kilichombo Isamilo Mwanza ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka vijana kuchangamkia fursa za utalii zilizopo mkoani Mwanza kwa kuanza kujifunza lugha mbalimbali za kigeni.

Mkurugenzi wa ICILD Charles Mwombeki akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Roberth Gabriel mara baada kutembelea Kituo Cha Kimataifa Cha Lugha ,Utamaduni na Mendeleo ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza wakazi wa Mwanza kujifunza Lugha za kimataifa ili iwe rahisi kuwasiliana na Watalii wanaoingia Jiji la Mwanza.

Mkurugenzi wa ICILD Charles Mwombeki akitoa hotuba kuhusu  Kituo Cha Kimataifa Cha Lugha ,Utamaduni na Mendeleo mbele ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Roberth Gabriel akiongea na wageni waliofika katika Kituo cha Kimataifa Cha Lugha ,Utamaduni na Mendeleo ambapo akipongeza kituo hicho kwa kufundisha Lugha zaidi ya 15 za Kigeni.

Raia wa Marekani na Mchumba wake ni miongoni mwa wanafunzi wa somo la Kiswahili katika Kituo Cha Kimataifa Cha Lugha,Utamaduni na Maendeleo akifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Binti Abela akitoa ushuhuda mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza namna Kituo Cha Kimataifa Cha Lugha ,Utamaduni na Mendeleo kilivyoweza kumsaidia kuongea Lugha ya Kingereza ambapo hivi sasa anauwezo mzuri wa kuongea Lugha hiyo.

No comments