Breaking News

Madaktari bingwa waweka kambi ya kutoa huduma mbalimbali kwa wagonjwa.

Katibu tawala Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike akiongea na Wananchi waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kambi ya madaktari bingwa iliyolenga kutoa huduma mbalimbali  ikiwemo vipimo

Na Hellen Mtereko Mwanza

Kambi  ya madaktari bingwa imezinduliwa leo Mkoani Mwanza katika hospital ya rufaa  sekou toure ilikuendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Zoezi hilo la uzinduzi wa kambi hiyo limezinduliwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza Samike  Ngusa amesema kuwa lengo la kambi hiyo ni kuwapatia matibabu wagonjwa wenye kipato cha chini ili waweze kupata ufumbuzi wa matatizo mbalimbali waliyonayo.

Ngusa amesema kuwa, ni furaha ya Serikali kuona wananchi wanapata matibabu na kuendelea na shughuli zao za kila siku na kuendelea kujitafutia kipato ambacho kinaiwezesha familia.

"Ninawapa pole nyingi wote wenye matatizo mbalimbali ya kiafya ambayo kwa sababu mbalimbali matatizo haya yalikuwa hayajapata ufumbuzi lakini mmekuja hapa leo ili mpate huduma ,niwatie moyo kuwahakikishia kuwa kuja kwenu hapa linakuwa na tija amesema Ngusa.

Amefafanua kuwa,wataalamu hao watatoa huduma kupitia kliniki  ambazo zimetengwa na watakuwepo  madaktari bingwa wa watoto, upasuaji ,magonjwa ya ndani,magonjwa ya moyo, kisukari ,shinikizo la juu na chini la damu,kinywa,saratani ya matiti na shingo ya kizazi na magonjwa ya kina mama na kizazi.

Hata hivyo amesema huduma hizo zinazotolewa kupitia kambi hiyo ifikapo mwaka  2022 zitaanza kutolewa katika jengo la mama na mtoto  lenye uwezo wa kubeba vitanda 261 na kwa sasa jengo hilo liko hatua za mwisho sanjari  na ununuzi wa vifaa.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa  Hospital ya Sekou Toure Bahati Msaki amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi ili kuja kupata matibabu kwani wamejipanga vizuri katika kutoa huduma hizo.

Msaki ameongeza kuwa wananchi wengi wanakuwa hawajitokezi pindi zinapotokea nafasi hizi za kuonana na madaktari bingwa na kuweza kufahamu matitizo yao hivyo wajiwekee utaratibu wa kuwa wanapata vipimo ili kuweza kugundua tatizo mapema.Mwishoooooo

No comments