Breaking News

Kusomesha watoto kumetajwa kuwa ni akiba

Mchungaji Dr Jacob Mutashi anayechunga kanisa la Kiloleli liliko Jijini Mwanza  akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuweka akiba

Na, Hellen Mtereko, Mwanza

watu wanaotaka kuwa na uzee mzuri wametakiwa kuwekeza katika kusomesha watoto ili waweze kuwasaidia pindi wanapozeeka kwani elimu ni akiba kuliko akiba yoyote.

Hayo yamesemwa na Mchungaji  Dr Jacob Mutashi, kutoka Kanisa la E.A.G.T lililopo kiloleli Jijini Mwanza wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuweka akiba.

Amesema kuwa kila unapopata pesa weka akiba pembeni kwanza kabla ya kuanza matumizi itakusaidia kukamilisha mipango yako uliyojiwekea ikiwemo kusomesha watoto.

"baadhi ya wazazi wamekuwa wagumu kwenye kuwekeza katika elimu hali inayopelekea kuishi maisha magumu baada ya kuzeeka hivyo jitahidini sana kuweka akiba hasa katika elimu", amesema



Mwishooo

No comments