Breaking News

URATIBU MBOVU WA KESI ZA WATOTO CHANZO CHA KUKOSEKANA KWA HAKI ZAO.

Na Tonny Alphonce,Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Roberth Gabriel amesema pamoja na Mkoa wa Mwanza kusimamia vizuri haki jinai lakini bado kunachangamoto upande wa mahabusu, undeshaji wa kesi, uratibu wa kushugulikia kesi za watoto na mahakama na hivyo kuwataka wajumbe wa Jukwaa la Haki Jinai kuhakikisha wanalitumia jukwaa hilo kutatua changamoto wanazokumbananazo wadau na jamii kwa ujumla.

Picha ya pamoja,Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Roberth Gabriel pamoja na wajumbe wa Jukwaa la Haki Jinai mara baada ya ufunguzi wa Jukwaa hilo mkoani Mwanza.(picha na Tonny Alphonce)

Mhandisi Roberth amesema kuna ukosefu wa uratibu mzuri wa kushunghulikia kesi za watoto na hivyo kesi nyingi za watoto huishia hewani na watoto wengi kukosa haki zao za msingi.

“Pamoja na kukosa uratibu wa kesi za watoto lakini tatizo lingine kubwa linalowaathiri watoto ni ucheleweshwaji wa upelelezi katika kesi nyingi za jinai hii hupelekea kesi nyingi kutofika mwisho”.alisema Mhandisi Gabriel.


Mhandisi Roberth Gabriel akizindua rasimi Jukwaa la Haki Jinai kwa Mkoa wa Mwanza.

Amesema kuzinduliwa kwa Jukwaa la Haki Jinai mkoani Mwanza kutatimiza matakwa ya sheria hivyo kuhakikisha mkoa unaendelea kusimamia vizuri huduma za haki jinai kwa makundi yoteJ

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Mkoa wa Mwanza Rehema Mkinze amesema kuzinduliwa kwa jukwaa hilo la haki jinai kutatua mashauri mbalimbali ya wananchi na kuwataka wananchi nao kuhakikisha wanarahisisha kazi ya jukwaa.

Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Mkoa wa Mwanza Rehema Mkinze akiongea na waandishi wa habari baada ya uzinduzi wa Jukwaa la Haki Jinai.

Amesema kwenye kesi za watoto ni jukumu la Ustawi wa jamii,Magereza,Mahakama,Polisi Pamoja na Jamii kushiriki kuona haki za watoto waliona kesi zinapatikana.

“Jamii ina jukumu la kutoa ushaidi kwaajili ya kesi kwenda vizuri na kuhakikisha haki inapatikana aidha kwa mtoto au kwa mtu mzima hivyo tunamatumaini kupitia hili jukwaa ambalo linamchanganyiko la wataalamu kutoka maeneo mbalimbali tunaona haki jinai itakwenda kupatikana.”alisema Rehema.

Amesema jukwaa hilo litakuwa na wajibu wa kutoa elimu pia kwa jamii hususani upande wa kesi za watoto kwa kuwa jamii pia inaonekana haijui kuhusiana na sheria ya Mtoto ambayo huelekeza usimamiaji wa kesi za watoto na namna zinavyotakiwa kuendeshwa na hukumu zao zinavyotakiwa kuwa.

Kuzinduliwa rasimi kwa Jukwaa la Haki Jinai mkoani Mwanza kutaharakisha utoaji wa haki mahakamani na kwa mahabusu.

No comments