Breaking News

WATOTO ZAIDI YA 50 WANA UTAPIAMLO MWANZA

 Na Annastazia Mginga,Mwanza

IMEELEZWA kuwa ukosefu wa usimamizi na uwandaaji wa vyakula vya watoto husababisha tatizo la utapiamlo.

Hali hiyo huchangiwa na majukumu utafutaji wa pesa na kushindwa kufuatilia masuala ya lishe Kwa watoto.

Akizungumza na MPC Blog Afisa Lishe wa Shirika la Baylor linaloshughurika na masuala ya lishe Kwa watoto Ester Msunga, kwenye uzinduzi wa miaka 50 ya hospitali ya Rufaa ya Bugando, amesema usimamizi wa uwandaaji wa vyakula katika familia umekuwa ni mdogo kwani wengi wao huachia wadada wa kazi.

Amesema lishe duni husabisha watoto kudumaa kimaumbile na kiakili hali inayofanya watoto kushindwa kukua vizuri .

"Ukosefu wa usimamizi mzuri wa kutoandaa vizuri vyakula vya lishe kwa watoto huchangia utapia mlo." Amesema Msunga.

Ameeleza kuwa kwa mwezi wanauwezo wa kuhudhmia watoto 50-60 wenye utapiamlo Kutoka sehemu mbalimbali ya Jiji la Mwanza.

Aidha ameeleza kwamba jamii imetakiwa kuelimishwa masuala ya lishe Ili kupunguza tatizo la utapiamlo kwa watoto.

Aidha kwa Mujibu wa utafiti wa kitaifa wa mwaka 2018 unaonyesha hali ya udumavu kitaifa ni silimia 30, huku mkoa wa Mwanza ukiwa na asilimia 29.3, ukondefu ukiwa asilimia 1.7.

Kwa upande wake Janeth Magori Mkazi wa Kiloleli amesema kuwa Serikali isichoke kutoa elimu ya lishe Katika ngazi za familia kwa kutumia wahudumu wa afya majumbani kwani baadhi ya wazazi hushindwa Kuandaa chakula vizuri kuhakikisha utapiamlo unapungua.

No comments