UZAZI WA MPANGO UNAPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO
Na Tonny Alphonce,Mwanza.
Wananchi wametakiwa kuendelea kutumia njia za uzazi wa
mpango kwa kuwa matumizi ya njia hizo yanapunguza vifo vya mama na mtoto kwa kiwango kikubwa.
Dk Mourice Amesema mama akizaa mfululizo bila
kupumzika anaweza kudhoofika kiafya lakini kuongeza nafasi ya kifo upande wake
au upande wa mtoto.
Dk Mourice amewataka wananchi waelewe kuhusu nia ya uzazi wa mpango ambayo haizuii idadi ya watoto wa kuzaa bali inasisitiza kuwepo kwa muda au nafasi kati ya mtoto mmoja na mwingine ili kutoa nafasi kwa mama kuimarika kiafya kutoka ujauzito mmoja kwenda mwingine.
‘Tukiangalia mitaani kwa Mwanza kuna watoto wengi
wa mtaani ambao wameshindwa kulelewa na familia kwa kukosekana kwa uzazi wa
mpango na kama jamii itatumia njia za uzazi wa mpango tunaweza kumaliza tatizo hili la watoto wa
mtaani’.alisema Dk Mourice.
Ester Ibrahimu afisa wa masoko Marie Stopes amewataka
wa kazi wa jiji la Mwanza kukitumia vema kituo hicho kipya kwa kuwa huduma
zimeongezeka upande wa mama na mtoto lakini pia kimeongezwa kitengo cha
mawasiliano kwaajili ya wateja watakao kuwa na maswali.
Aidha Ester amesema kituo sasa tayari kina madaktari
bingwa wa wanawake na watoto ambao watawahudumia kwa ukaribu wanawake na watoto
na hivyo kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika kutokana na matibabu sahihi
kwenda kwa mgonjwa.
Lidya Mashauri mkazi wa Mkuyuni jijini Mwanza ameshukuru kwa huduma za bure zinazotolewa wiki hii na shirika hilo hasa upande wa magonjwa ya kina mama na watoto na kuwataka wanawake kujitokeza ili waweze kupima afya zao.
Amesema ni wazi kuwa kina mama mara nyingi ndio hupata
changamoto za kiafya hasa kipindi cha uzazi hivyo ni vizuri kutumia wiki hii ya
matibabu bure kufanya uchunguzi wa afya zao.
No comments