Breaking News

Wataalam wa afya watakiwa kulinda vifaa tiba


Dk Dorothy Gwajima wapili(kulia) mwenye koti jekundu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya  wataalamu wa mionzi

Na Hellen Mtereko,Mwanza

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk Dorothy Gwajima amewataka watalaam wa Afya nchini kulinda vifaa tiba vya vipimo mbalimbali ili vidumu kwa nda mrefu.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Mwanza na Dk Gwajima kwenye kikao cha kufunga Kongamano la siku tatu lililowakutanisha watalaamu wa Chama cha mionzi Tanzania (TARA) kujadili mambo yanayohusiana na utendaji kazi wao.

Amesema baadhi ya watalaam wa Afya wamekuwa na matumizi mabovu ya vifaa tiba na kusababisha uharibifu ambao huligharimu taifa fedha nyingi na kuleta usumbufu kwa wagonjwa kutopata tiba kwa wakati.

"Kifaa kinaharibika lakini hakuna taarifa ya nini kimesababisha uharibifu huo na wala hakuna maelezo ya kiasi gani cha fedha imeingiza huo utaratibu hautakiwi" alisema Dk Gwajima.

Waziri amewataka watalaam hao kutunza vifaa hivyo kama ambavyo wanafanya kwa vitu vingine vilivyo na umuhimu mkubwa kwao Ili viweze kusaidia wagonjwa katika matibabu yao kwa muda mrefu sanjari na  taarifa ya matumizi ya vifaa hivyo kufanywa  kila siku.

Amewataka watalaam hao wajitume na kufanya kazi kwa bidiii na ushirikiano kwa kuzingatia weledi wa maadili ya taaluma yao Ili iweze kuleta tija kwa taifa.

Rais wa TARA Bakari Msongamwanja ameomba serikali kuendelea kutoa ushirikiano Ili sekta ya taaluma ya mionzi ipanuke na kuweza kufikia maeneo mengi kwani vituo vya Afya vimeongezeka.

Amesema serikali iongeze jitihada za kuajiri watalaamu wa mionzi Ili waweze kwendana na wingi wa vituo vya afya vilivyopo hapa nchini.

Mwishooo

No comments