Breaking News

UKATILI KWA WATOTO BADO NI TATIZO KANDA YA ZIWA

 Na Annastazia Maginga, Mwanza.

Imeelezwa kuwa  uelewa wa kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto bado ni changamoto Katika mikoa ya Kanda ya ziwa Kutokana na tatizo hilo kushamili ukilinganisha na Mikoa mingine ya Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na Wananchi pamoja na wadau wa kupinga vitendo vya ukatili Kwa watoto 

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya 16 ya kupinga ukatili Kwa watoto na wanawake yaliyofanyika kitaifa Jijini Mwanza Mkuu wa Mkoa Mhandisi, Robert Gabriel amesema Kanda ya ziwa inaongoza kwa vitendo ya ukatili dhidi ya watoto.

Aidha licha ya kuwepo kwa uelewa mpana Katika jamii kuhusu kufichua vitendo vya ukatili Kwa watoto lakini bado vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka kila mwaka.

Mkoa wa Shinyanga umetajwa kuwa na asilimia 78, ukifuatia na Mkoa wa Mara asilimia 78 hatua iliyopelekea kufanyika Kwa maadhimisho hayo na kutoa Elimu Kwa Wananchi Ili kuhakikisha vitendo hivyo vinakoma.

"Mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa asilimia 78, ikifuatiwa na Mkoa wa Mara asilimia 78,Kagera asilimia 67, Geita asilimia 63, Simuiyu asilimia 62 na Mwanza asilimia 60" amesema Mhandisi Robert.

Aidha uelewa uliojengeka Kwa wakazi wa Jiji la Mwanza kuhusu kufichua vitendo vya ukatili. 
Watoto wa Shule ya Msingi Mitindo Wilaya ya Misungwi    wakitumbuiza ngonjera yenye ujumbe wa kukomesha matukio ya vitendo vya ukatili Kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel. 

Umeongezeka Kutoka matukio 205 ya mwaka 2019 hadi 305 mwaka 2021 Wilaya ya Magu huku Misungwi ikiwa na matukio 189 ya mwaka 2019 hadi 220 mwaka 2020.

Kwa upande wake msemaji wa dawati la jinsia Kutoka Jijini Dare Salaam ACP Faidha Suleiman ameeleza kuwa wameanza kutoa Elimu ya kufichua vitendo vya ukatili Kwa Wananchi baada ya idadi ya vitendo hIvyo kuongezeka Katika maeneo ya Jiji la Mwanza.

"Tumeamua kufanya maadhimisho haya Jijini Mwanza Kutokana na vitendo vya ukatili kushamili Katika mikoa ya Kanda ya ziwa hata hivyo Serikali imetunga sera ya maendeleo ya mtoto ya mwaka 2009 na Sheria ya makosa ya kujamiana Ili kulinda utu wa watoto" amesema ACP Faidha.
 
Hata hivyo amesema kuwa ufanikishaji wa kesi za ukatili ni mdogo licha ya kutoa za uwepo wa vitendo hivyo na kwamba wanachi wafike Katika dawati la jinsia kufika kutoa taarifa za ukatili dhidi ya watoto.

No comments