Breaking News

NSSF WAIPONGEZA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MWANZA

Na Tonny Alphonce,Mwanza

Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa amezitaka Taasisi mbalimbali zilizopo Kanda ya Ziwa kujitokeza kushiriki katika Usiku wa Wadau Wa Habari ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi Wa Habari  Mkoa wa Mwanza.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa akizungumza na wanahabari ofisini kwake kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na NSSF Mwanza.

Akizungumza na Waandishi Wa Habari ofisini kwake Leo tarehe 30/05/2022,Kahensa amesema usiku huo wa kuwakutanisha wadau Wa Habari ni mzuri Kwa kuwa inatoa nafasi kwa taasisi au shirika kuzungumzia kazi wanazofanya mbele ya Vyombo mbalimbali vya habari na matokeo yake habari hiyo huenda mbali zaidi.

"Binafsi niwapongeze sana Mwanza Press Club kwakuwa mmekuwa mkisaidia kufikisha elimu kwa wanachama wetu wengi kupitia huu Usiku wa Waandishi Wa Habari na Wadau".alisema Kahensa.

Akizungumzia huduma mbalimbali  wanazozitoa,Kahensa amesema wanachama wa NSSF wamekuwa wakinufaika na mafao 7 likiwemo Fao la Uzazi,Fao la Kifo,Fao la Kutokuwa na Ajira,mafao ambayo yamekuwa msaada mkubwa Kwa wanachama.


Usiku wa Waandishi na Wadau Wa Habari Kanda ya Ziwa unatarajiwa kufanyika tarehe 03/06/2022 katika ukumbi wa Rock City Mall ambapo hadi sasa wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki.

No comments